Mauzo Ya Kampuni Ya Apple Yashuka Kwa Kasi Sana

Soko la thamani la kampuni ya Apple limeshuka sana. Siku ya Jumatatu (Machi 23) kampuni hiyo imetangaza kuwa kwa sasa haina thamani ya ($1 Trillion) tena ikiwa ni mara ya kwanza tangu mwezi Septemba mwaka jana.

Kufuatia janga la ugonjwa wa Corona, Kampuni hiyo imekumbwa na anguko kubwa la mauzo nchini China na imefunga maduka yake mengi duniani kote.

Mwezi August 2018, Apple ilikuwa kampuni ya kwanza duniani kuwa na thamani ya ($1 Trillion) Kuanguka kwa Apple kumeiacha Microsoft kama kampuni pekee ya nchini Marekani ambayo ina thamani hiyo.


EmoticonEmoticon