Mgonjwa Wa Corona Apona Kenya Huku Wengine Watatu Wakiripotiwa Na Mishahara Rais, Naibu Na Mawaziri Ikipunguzwa


Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ametangaza kuwa mtu wa kwanza amepona kabisa ugonjwa wa corona, huku wagonjwa watatu wakiripotiwa zaidi.
''Hii inamaanisha kuwa ugonjwa huu unaweza kukabiliwa''alisema rais Kenyatta katika hotiba yake kwa taifa.
Idadi ya walioambukizwa ugonjwa wa corona nchini Kenya imefikia 28.
Rais pia ametangaza hatua kadhaa ambazo zitasaidia serikali yake kukabili janga la corona ikiwa ni pamoja na amri ya kutotoka nje kuanzia Ijumaa Machi 27 kuanziasa moja usiku hadi saa kumi na mbili asubuhi.
''Orodha kamili ya watu wanaotoa huduma muhimu ambao hawatathiriwa na amri hio itatolewa na wizara ya ya usalamma wa ndani'' alisema rais Kenyatta.
Ushuru wa ziada utapunguzwa kutoka asilimia 16% hadi 14% kuanzia Aprili 2020.
Rais ametangaza hatua ya kupunguza mshahara wake kwa asilimia 80 huku mawaziri wake wakipunguza mshahara wao kwa asilimia 30.
Rais na naibu wa rais wamekubali kupunguza asilimia 80 ya mishahara yao kwa hiari huku mawaziri na makatibu wa kudumu wakikubali kupunguziwa asilimia 30 ya mshahara wao kwa asilimia 30.
credit:bbc


EmoticonEmoticon