Mhubiri Ataka Sadaka Itumwe Kwenye Simu Kama Watu Hawafiki Kanisani, Afungua Whatsapp Group Kwaajili Ya Waumini Wake

Mhubiri mmoja mmoja wa kanisa la The blessed  Chosen huko Bomet nchini Kenya ameamua kutengeza kundi la whatsapp la waumini wake wote kwa lengo la kuhakikisha kwamba kila mmoja analipa sadaka licha ya kukosa kwenda kanisani .

Mhuburi huyo amesema kwa sababu ya agizo la serikali kuwazuia  watu kukongamana makanisani , lazim kila muumini ahakikishe kwamba anatuma sadaka yake kila jumapili endapo haitawezekana watu kwenda kanisani.

Josephat Korir ameandika majina ya wote waliotuma  sadaka zao jumapili iliyopita na kuwataka wale ambao hawakuenda kanisani kutuma pesa hizo kwa nambari yake . 

Hatua hiyo imewashangaza waumini wake ambao baadhi yao wametoka kwenye kundi hilo la whatsapp.

Katika ujumbe wake mkali kuhusu umuhimu wa kutoa sadaka ,Korir alionya kwamba watakaokosa kutoa michango yao wasilitarajie kanisa lake kuwapa usaidizi wowote au kujihusisha na mambo yao kama vile harusi ,maazishi na kubatizwa .

Wengi walionekana kupuuza tisho lake  huku wakisema wako tayari kulihama kanisa hilo kwani makanisa ni mengi .

Korir  katika ujumbe wake alisema sadaka ni muhimu ili kuendeleza oparesheni za kanisa lake na waumini walifaa kutii ushauri wake .

Wengi  katika sehemu hiyo wanangoja kwa hamu kuona mambo yatakuaje katika kanisa hilo wakati tutakapomaliza vita dhidi ya virusi  vya Corona .
credit:radiojambo


EmoticonEmoticon