Mike Tyson Kwake Ni Bora Kifo Kuliko Kuishi

Bingwa wa zamani wa ndondi za uzito wa juu duniani, Mike Tyson amesema anasubiri kwa hamu kifo chake kwa kuwa “kuishi kunaweza kuwa ni kugumu kuliko kufa.”

Tyson mwenye umri wa miaka 53, alisema katika mahojiano na tovuti ya The Sportsman ya Uingereza kwamba anaamini kutoogopa kwake jambo lolote kulimfanya awe tayari kwa kifo ulingoni ingawa aliamini ni yeye ndiye angeua kama kungetokea kifo katika moja ya mapambano yake.

“Nilijua kwamba kuna uwezekano wa mimi kufa wakati wa mazoezi au wakati wa pambano, lakini sikuwa na hofu yoyote kwa kuwa niliamini kwamba kama kuna mtu angekufa, ni mimi ndiye ningeua. Kujiamini huko kulikuwa ni mbinu ya kujinusuru.
“Lakini sasa, kutokana na uzoefu na kutokana na kile ninachoamini, kila ninapofahamu zaidi kuhusu kutokuwepo duniani ndipo ninapokuwa tayari zaidi kufa.”

Alipoulizwa endapo ni kweli anasubiri kifo chake kwa hamu, mbabe huyo wa “knockout” alisema: “Ndio, siogopi. Kuishi kunaweza kuwa ni kugumu kuliko kufa. Ndivyo ninavyoamini. Sijui kama ni kweli. Kwa sababu kuishi kunahitaji ujasiri. Bila ujasiri, huwezi kumudu kuishi.

“Maisha ni safari, maisha ni mapambano. Watu wana kila kitu, lakini bado maisha yanakuwa magumu kwao,” alisema Tyson.


EmoticonEmoticon