Mtoto Wa Mfalme Asema Hajawahi Kufikiria Kumwomba Pesa Trump Kwani Pesa Kwao Sio Tatizo

Baada ya Mwanamfamle Harry wa Uingereza kutangaza kuhamia nchini Marekani wakitokea Canada ambao waliondoka kwenye Jumba la Kifalme na kwenda kuanza maisha mapya Canada na sasa wanataka kuhamia Marekani, Trump amewataka wajilipie ulinzi wenyewe.
Rais wa Marekani ametumia ukurasa wake wa Twitter na kuandika ujumbe kama huu.
“Mimi ni rafiki wa Malkia, nampenda na naipenda Uingereza, iliripotiwa kuwa Mwanamfalme Harry na Mkewe Meghan ambao waliondoka kwenye Jumba la Kifalme wataishi Canada, sasa hivi wameondoka Canada eti wanakuja Marekani, waje lakini wajue Marekani haitolipa gharama za ulinzi, watajilipia wenyewe”.
Mwanamfalme Harry na Mkewe Meghan wamesema hawana mpango wa kuiomba Marekani iwalipie ulinzi na kumtaka Trump ambaye amesema hatowalipia, aondoe wasiwasi”pesa kwetu sio tatizo, mipango yote ya ulinzi tukiwa Marekani imeshafanywa, hatujawahi hata kufikiria kuomba pesa kwa Trump”


EmoticonEmoticon