R Kelly Apeleka Maombi Mahakamani Yanayohusiana Na Corona

R Kelly ameiomba mahakama kumuachia kwa muda ili kujilinda na maambukizi ya virusi vya CORONA ambavyo vinaitikisa Marekani kwa sasa.

Kwenye shauri ambalo lilifunguliwa jana Alhamis, Mwanasheria wa R. Kelly amemuomba Jaji Harry Leinenweber kupeleka mbele maombi ya kusikiliza dhamana ya mteja wake, badala yake imuachie kwa muda kutokana na hofu ya kupata virusi vya ugonjwa wa CORONA kwani jela kuna mwingiliano mkubwa wa watu.

R. Kelly bado anasubiri kusikilizwa kwa mashtaka yake zaidi ya 10 ya Unyanyasaji wa Kingono.


EmoticonEmoticon