Shirika La Afya Duniani Lawaonya Vijana Dhidi Ya Ugonjwa Wa Corona

Vijana hawana kinga ya mwili dhidi ya coronavirus na wanapaswa kuepuka kuepuka mikusanyiko ya kijamii na kuwaelezea wazee na watu wengine wanaokabiliwa na hatari ya maambukizi juu ya virusi hivyo , limeonya shirika la Afya Duniani (WHO)
Chaguo lililofanywa na vijana linaweza kuwa "tofauti kati ya maisha na kifo cha mtu fulani", Mkurugenzi Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema.
Zaidi ya wagonjwa 11,000 yatari wamekwishafariki duniani kutokana na Covid-19 ambao ni ugonjwa unaoshambulia mfumo wa kupumua.
Kwa ujumla takriban wagonjwa 250,000 wamepatikana na virusi vya corona.
Tamko la Mkuu wa WHO linafuatia taarifa kuwa vijana katika nchi nyingi wamekua wakipuuza tahadhari za kiafya zinazotolewa kuhusu coronavirus katika nchi zao , kwasababu uapatikanaji wa virusi hivyoumekua ni miongoni mwa watu wenye umri mkubwa zaidi.
Milipuko wa coronavirus ulirekodiwa kwa mara ya kwanza nchini Uchina mwezi Disemba. Lakini kwa sasa kitovu cha janga hilo ni Ulaya.
Nchini Italia-ambako virusi vimewauwa watu zaidi ya nchi nyingine - idadi ya vifo imefikia hadi watu 627 siku ya Ijumaa, na hivyo kufikia jumla ya vifo 4,032, na kuifanya kuwa ndio siku ya vifo zaidi kuwahi kushuhudiwa katika nchi moja tangu mlipuko huo uanze.


EmoticonEmoticon