Vyakula Ambavyo Havistahili Kuliwa Kwa Wingi Ambvyo Husababisha Magonjwa Kwa Haraka

Awali ya yote elewa tu kuwa hii ni orodha ndogo sana katika vyakula ambavyo mwanaume hatakiwi kutumia kwa wingi. Ni sehemu ndogo na kwa hakika vinazidi zaidi ya vyakula 20 ambavyo wanaume hawatakiwi kuvupa kipaumbele katika lishe.

Ukiacha sigara ambayo imeandikwa wazi ni hatari kwa afya yako, vitu vingi tunavyokula na kunywa havifai kwa afya zetu.

1. Punguza kula vyakula feki kuzuia kupoteza nywele
Moja ya matatizo makubwa upande wa urembo kwa wanaume ni kupoteza nywele (upara).
Lakini kama unatafuta kitu cha kukilaumu dhidi ya tatizo lako la kunyonyoka nywele basi ni hiyo sahani yako ya chipsi unayokula kila siku.  
Vyakula feki (junk foods) ni hivyo vinapatikana kwenye fast foods na takeaway centers nyingi hasa mijini kadharika vyakula vile vyote vya kwenye maboksi.
Vyakula hivi feki vina kiasi kingi mno cha lehemu (cholesterol) na lehemu hii hupelekea kile huitwa kwa kitaalamu kama ‘pregnenolone’ na kupelekea kiasi kikubwa cha ‘dihydrotestosterone’ (DHT) na hatimaye kupotea kwa nywele kichwani a.k.a upara.
2. Punguza kunywa pombe au acha kabisa kuzuia kuota matiti
Wanaume wengi wanaokunywa bia kupita kiasi huwa na uwezekano mkubwa wa kupatwa na tatizo la kuota matiti kama wamama tatizo lijulikanalo kwa kitaalamu kama ‘gynecomastia’.
Kwenye bia au pombe mara nyingi hakuna lishe ya moja kwa moja na hivyo hukufanya ujisikie njaa au hata kuongzeka kwa njaa zaidi na ndiyo sababu unaambiwa kama huna uhakika utakula wapi ni bora usinywe pombe ili kulinda afya yako.
Kwenye bia kuna kitu kama homoni ya oestrogen ya kupandikizwa na hivyo unywaji pombe kupita kiasi kuna uhusiano wa moja kwa moja na matokeo ya wanaume kuwa na matiti kama wanawake.
3. Acha kutumia baadhi ya mafuta ya mboga mboga kuepuka saratani ya tezi dume
Mafuta yatokanayo na mboga mboga au mimea yamekuwa yakipigiwa debe kwa miaka mingi na watu wanaojihusisha na lishe, wajasiriamali wa mafuta hasa ya alizeti na wale wanaharakati wenye hasira sana na mafuta yatokanayo na wanyama.
Kama kuna orodha inayoshtua watu wengi basi ni hili la mafuta ya mimea au mboga mboga. Watu wengi wanaona haiwezekani na wengine wanafikia hatua ya kuhoji maswali ambayo yanakatisha tamaa na hasa wajasiriamali wa alizeti.
4. Popcorn
Popcorn au bisi ni chakula kingine mwanaume hatakiwi kula, hupikwa kwa kutumia mafuta yasiyo na afya, sodiamu nyingi na ni chanzo cha baadhi ya kansa.
Kuna kitu kinaitwa ‘Diacetyl’ kinachopatikana kwenye popcorn ambacho kinahusika na kusababisha kansa na kuna kingine kiitwacho ‘Perfluorochemicals’ ambacho huathiri tezi ya thyroid na ugonjwa wakati huo huo husababisha ugonjwa wa kupungukiwa umakini ujulikanao kwa kiingereza kama ‘Attention-deficit/hyperactivity disorder (ADHD)‘.
5. Mkate mweupe
Mkate mweupe una wanga mwingi zaidi usio na faida. Kwenye hatua za kutengeneza mkate mweupe vitamini zote za kundi B hupotea, hupotea pia nyuzinyuzi (fiber).
Siyo hivyo tu mkate mweupe umesemekana kuwa ni sababu ya ugonjwa wa kisukari na kuongeza uzito zaidi mwilini wakati huo huo ukisababisha tatizo la kufunga choo au kupata choo kigumu sana.
Vingine vinavyofanana na na hilo ni ugali wa sembe, tambi nyeupe, chai ya rangi na kahawa.
Kula mkate ambao ngano yake haikukobolewa (brown bread), kula ugali wa dona na chai unaweza kutumia tangawizi au mdalasini badala ya majani ya chai.
6. Chumvi ya mezani
Chumvi ya mezani ile ya unga nyeupe haifai kwa mwanaume. Kila mmoja amesikia chumvi hii husababisha shinikizo la juu la damu na pamoja na hayo bado sehemu kubwa ya watu wanatumia chumvi hii.
Chumvi ya mezani husafishwa kwa kuondoa madini madini na hupitishwa katika joto la nyuzi joto 1093.
Kwa hiyo uliyonayo sasa ni asilimia 40 ya sodiamu na asilimia 60 ya kloridi, na kisha kemikali kama vile ‘aluminium silicate’ huongezwa ili kuifanya isishikane na hivyo kubaki katika hali ya unga.
Aluminium silicate ni sumu kali inayoharibu mfumo wetu wa fahamu. Inatajwa kuwa ni miongoni mwa sababu zinazosababisha ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu (Alzheimer).
Chumvi ya mawe ya baharini ile ambayo haijapita kiwandani (unrefined sea salt) ndiyo nzuri zaidi kwa afya ya mwanaume.


EmoticonEmoticon