Wahubiri Walalamikia Kiasi Kidogo Cha Michango Makanisani Kwaajili Ya Coronavirus

Baadhi ya wahubiri kutoka Baringo nchini Kenya wamelalamika kuhusu kiasi kidogo cha fedha walizochangisha kama sadaka  baada ya waumini wengi kusalia nyumbani bila kwenda kanisani kwa ajili ya hofu ya virusi vya Corona.

Kasisi wa wa kanisa la  Full Gospel Churches of Kenya (FGCK)- mjini Kabarnet Daniel Chemon amesema idadi ya waliohudhuria misa ilipungua kabisa siku ya jumapili.

Alisema kanisa hilo huwa na watu wengi sana siku za jumapili lakini  siku ya jumapili machi 22 hali haikuwa kama kawaida. Anasema pia walilazimika kuharakisha programu za kanisa.

Kwa ajili ya idadi ndogo ya waumini waliokwenda kanisani amesema kiasi cha michango iliyotolewa kama sadaka kilikuwa cha chini sana  na hali hiyo iliripotiwa katika makanisa yao yote  kwenye kaunti nzima.
credit:radiojambo


EmoticonEmoticon