Waziri Mkuu Wa Uingereza Athibitisha Kuwa Na Corona (VIDEO)

Bwana Johnson amekutwa na coronavirus, baada ya kufanyiwa vipimo, imesema ofisi yake Downing Street.
"Nimekuwa na dalili ndogo za coronavirus, ambazo ni viwango vya juu vya joto la mwili na kikohozi ambacho hakikomi ," Bwana Johnson amesema katika video aliyoituma kwenye ukurasa wake Twitter.
Waziri Mkuu huyo wa Uingereza amesema kuwa ataendelea kulingoza taifa kutoka nyumbani baada ya kupatikana na Covid-19.
Bwana Johnson atajitenga binafsi - katika makao yake ya kikazi ya Downing Street, baada ya kupimwa na kupatikana na virusi hivyo na muhudumu wa huduma za afya nchini Uingereza katika ofisi yake al maarufu No 10.
Bado ataendelea kuwa mkuu wa shughuli za kukabiliana na mzozo wa coronavirus, kulinga na taarifa iliyotolewa na ofisi yake.
"Ninafanyakazi kutoka nyumbani na nimejitenga. Hilo ndio jambo sahihi la kufanya''.
"Ninaweza kuendelea, nashukuru teknolojia kwamba ninaweza kuwasiliana na viongozi wakuu na kuongoza taifa dhidi ya virus.", amesema.
" Kwa hiyo nashukuru sana kwa kila mtu anayefanya kile ninachokifanya, kufanya kazi kutoka nyumbani ili kuzuwia maambukizi ya virusi kutoka nyumba moja hadi nyingine'', aliongeza.
" Hivyo ndivyo tutakavyoshinda."


EmoticonEmoticon