Alilolizungumza Ronaldinho Katika Mahojiano Ya Kwanza Toka Atoke Jela

Ronaldinho amefanya mahojiano kwa mara ya kwanza toka akamatwe nchini Paraguay kwa tuhuma ya kukutwa na passport bandia.
Ronaldinho ,40, katika mahojiano maalum na chombo cha habari cha ABC cha Paraguay amefunguka na kueleza kuwa hakujua kama Passport aliyokuwa nayo ni bandia na endapo siku akachiwa uhuru wake kitu cha kwanza atambusu mama yake kwa furaha.
”Kuanzia sasa na kuendelea kushirikiana na Mahakama kutoa ufafanuzi kuhusiana na hili, nina imani na siku zote nimekuwa nikisali mambo yatakuwa sawa na Mungu atasaidia kumalizika hivi punde”
”Nilipogundua kuwa naenda gerezani iliniumiza sana, sikuwahi kuwaza nitakuja kuwa katika hali kama hii, katika maisha yangu yote nimejaribu kwa kiwango cha juu kuwapa watu furaha kupitia soka langu”
Hadi sasa Ronaldinho na kaka yake wapo nje kwa dhamana Paraguay wakiwa katika hoteli maalum ya nyota nne chini ya uangalizi mkali ili wasitoroke.


EmoticonEmoticon