CORONA : Idadi Mpya Ya Wagonjwa Tanzania 306, Waliopona Wafikia 84

Wizara ya Afya Zanzibar imetoa taarifa ya ongezeko la Wagonjwa wapya saba wa corona na kufikisha idadi ya wagonjwa 105 kutoka 98, wagonjwa wote wapya ni Raia wa Tanzania na wametokea Unguja, kwa ongezeko hili sasa idadi ya visa vya corona Tanzania nzima imefikia 306 kutoka 299.

Wagonjwa 36 wa corona wamepona na kuruhusiwa kwenda nyumbani huku wakishauriwa kubaki katika nyumba zao kwa siku 14 kabla ya kurudi kwenye shughuli zao, kwa ongezeko hili sasa idadi ya waliopona corona Tanzania nzima imefikia 84 kutoka 48.


EmoticonEmoticon