CORONA : Kenya Yasajili Visa 14 Jumla 172. Idadi Ya Waliopona Ni Watu Saba

Siku nyingine tena ambapo taifa la Kenya limesajili visa vingi vya watu walioathirika na virusi vya Corona katika bara la Afrika Mashariki na hii leo,waziri wa afya Mutahi Kagwe amedhibitisha kuwa watu 14 zaidi wamepatikana na virusi vya Corona ,kufikisha idadi ya watu walioambukizwa nchini kuwa 172.


Kwa sasa Mutahi amesema watu 3 wameruhusiwa kutoka kwa hospitali na kufikisha idadi ya watu 7 waliopona.


Watu hao 14 ,12 ni wakenya na 2 kutoka mataifa ya kigeni. Chini ya masaa 24 ,watu 696 wamefanyiwa vipimo.

Kati ya watu hao 14 ,7 ni kutoka kaunti ya Nairobi, 2 Mombasa, 1 Kiambu, Mandera 2 ,Machakos 1 na Kisii 1.


Nairobi – 7 Mombasa – 2 Machakos – 1 Kisii- 1 Kiambu – 1 Mandera- 2.


Vilabu vya Gofu nchini vimefungwa na waziri wa Afya Mutahi Kagwe ambaye amesema kuwa ni kutokana na idadi kubwa ya watu wanaojumuika eneo la vilabu hivyo ,ikiwa ni hatari haswa wakati huu ambapo taifa la Kenya linakabiliana na virusi vya Corona.


Wakati uo huo Mutahi amesema maafisa wote wa afya wanaohudumu katika hospitali ambazo waathiriwa wametengwa ni sharti waanze kufanya vipimo vya matibbabu.


Wananchi waliokatika kaunti zilizoathirika wataanza kufanyiwa vipimo. Usajili wa watu na hoteli nchini umesitishwa na Serikali.
Credit:Radiojambo


EmoticonEmoticon