CORONA : Sababu Za India Kuvikataa Vifaa Vya Vipimo Kutoka China, Dosari Iliyogundulika

India imesitisha uagizaji wa karibu vifaa nusu milioni vya kupimia virusi vya corona kutoka China baada ya kubainika kuwa vifaa hivyo ''Vina dosari''.
Mji wa Delhi pia umeondoa vifaa ambavyo tayari vilikuwa vinatumika katika majimbo kadhaa.
Vifaa hivyo huchukua muda wa karibu dakika 30 kutoa majibu. Hutumiwa kusaidia maafisa kuelewa hali ya maambukizi katika eneo fulani.

China imekasirishwa na madai ya India.
''Ubora wa vifaa tiba kutoka China ni jambo linalopewa kipaumbele. Si haki kwa watu fulani kuita vifaa vitokavyo China kuwa vyenye ''dosari'' alieleza msemaji wa ubalozi wa China Ji Rong katika taarifa yake siku ya Jumanne.
Vifaa hivi vya upimaji haviwezi kupima virusi vya corona vyenyewe na wanasayansi kadhaa wameeleza kuhusu matumizi yake katika kubaini ugonjwa.
Majimbo kadhaa nchini India yamekuwa yakishinikiza baraza la utafiti(ICMR) nchini humo kuruhusu vipimo kwa kutumia vifaa hivyo kutokana na madai kuwa India haifanyi jitihada za kutosha.
Credit:bbc


EmoticonEmoticon