CORONA : Utaratibu Mpya Uliowekwa Na Raisi Wa Uganda Kwa Madereva Wa Magari Makubwa Ya Mizigo

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametangaza hatua mpya za kudhibiti mienendo ya madereva wa malori yanayoingia nchini humo kutoka mataifa jirani baada ya zaidi ya madereva 20 kupatikana na ugonjwa wa Covid-19.
Hatua hizo ni pamoja na kila lori kuwa na mtu mmoja - dereva pekee yake ambaye hataruhusiwa kulala hotelini wala nyumbani kwa watu. Bw. Museveni pia amesema mienendo ya madereva hao itachunguzwa
Katika hotuba yake kwa taifa usiku wa Jumanne Rais Museveni pia aliangazia kuongezeka kwa chuki dhidi ya madereva hao kutoka kwa baadhi Waganda ambao wanahofia wataleta maambukizi ya corona niching humo.
Museveni aliongeza kwamba kusitisha usafirishaji wa bidhaa itakuwa na athari kubwa lakini alikubali kuwa madereva hao ni tishio katika mapambano ya nchi hiyo dhidi ya corona ikitoa mfano wa janga la Ukimwi la miaka ya 1980 na miaka ya tisini wakati ambapo madereva wa malori katika kanda hiyo waliaambukiza watu virus vya HIV katika kila miji waliyopitia wakiwa safarini.


EmoticonEmoticon