CORONA : Wabunge Wapatikana Na Ugonjwa Kenya Huku Vikao Vya Bunge Vikifutwa

Kimezuka kizaazaa bungeni baada ya kuibuka ripoti kwamba wabunge 17 wameambukizwa  virusi vya corona .

Kwa mujibu wa taarifa za kuaminika katika wizara ya afya  ,maspika wa mabunge yote walishauriwa kufutilia mbali vikao vya mabunge yote  kwa sababu ya wabunge walipatikana na virusi hivyo . 

Baadhi yao walipimwa wiki jana na matoeo ya vipimo hivyo yalitolewa sik ya jumatatu  na kuzua hofu katika mabunge yote .

“ Wanashuku wabunge 17 wana virusi hivyo na ndio kwa sababu vikao vya mabunge yote vilisistishwa .tunangoja maelezo kamili’ amesema mbunge mmoja hakutaka kutajwa. Majina yao kwa sasa hayawezi kutajwa kwa sababu  ni hatia kufichua hali ya kiafya ya mtu bila idhini yake .

Seneta mmoja amesema spika alitangaza kusitishwa kwa vikao vya bunge ili kuzuia kuambukizwa kwa wabunge na masenata zaidi  endapo  walioambukizwa virusi hivyo wangeruhusiwa  kutangamana na wenzao katika bunge .

Maseneta ,wabunge na wafanyakazi wa bunge wamekuwa  wakipimwa kwa hiari kujua iwapo  wana ugonjwa huo  katika majengo ya bunge  tangu wiki jana . 

Zaidi ya wabunge 200 na maseneta  wakiwemo maspika wa mabunge yote wamepimwa virusi hivyo na wameanza kupokea matokeo yao kila mmoja .

Hata hivyo spika wa senate Ken Lusaka  amekanusha uvumi huo akisema ni vigumu kujua ni nani ana virusi hivyo kwani kila mtu alipokea matokeo yake kivyake .

Baadhi ya wabunge ambao wamejiweka katika karantini wenyewe ni   mbunge wa Eldas Adan Keynan, Naomi Shaban (Taita Taveta), Aaron Cheruiyot (Kericho)  na George Khaniri (Vihiga).  Walikuwa wamesafiri kwenda Uingereza mapema mwezi uliopita .
Credit:Radiojambo


EmoticonEmoticon