Diamond Platnumz Afunguka Hoteli Yake Mpya Pamoja Na Gari Jipya Aina Ya Rolls Royce Aliyonunua


Kupitia kipidi cha Good morning kinachoruka Wasafi Fm Diamond amefunguka kuhusiana na Hoteli aliyonunua ameneo ya Mikocheni na kusema kuwa, "Nimenunua Hoteli maeneo ya Mikocheni na nimeshakabidhiwa Documents zangu na ipo kwenye marekebisho kadhaa kisha nitaitambulisha.

Na Hoteli hiyo ambayo nimeinunua niko radhi niitoe kwa serikali muda huu ili iweze kutumika kama karantini au hospitali mpaka pale Corona itakapoisha".
Kwa upande wa gari aina ya Rolls Royce inayozagaa mitandaoni ambayo inasemekana alinunua amefunguka hilo na kusema kuwa, "Namshukuru rafiki yangu ambaye yupo London, ndiye aliyenisaidia kukamilisha ndoto yangu ya kununua gari aina ya Rolls Royce, Japo ile inayozagaa mitandaoni sio hiyo, niliyonunua ipo tofauti kabisa".


EmoticonEmoticon