Documentary Ya Kitabu Cha Michelle Obama Kuletwa Na Netflix, Tazama Trailer

Huwenda wewe ni mingoni mwa waliopata nafasi ya kukisoma kitabu cha Michelle Obama "Becoming" ambacho kilikamata rekodi ya mauzo mwaka 2018.

Baada ya Michelle kukiachia kitabu hicho, aliamua kufanya ziara katika miji 34 ambapo alitoa hotuba na maneno ya kuhamasisha watu kuwa wanachotaka. Wakati akipita huko kulikuwa na camera zikimfuata kila eneo na leo hii kampuni ya Netflix imetangaza kuja na Documentary.

Tayari wameachia trailer, na inaonesha kwamba Documentary hiyo itahusu mambo yote ambayo yalitokea wakati wa ziara ya Michelle kwenye miji hiyo 34.


EmoticonEmoticon