Godoro Analolalia Drake Lenye Thamani Zaidi Ya Tsh. Million 900

Kwenye mahojiano na jarida la Architectural Digest, Drake alisema Chumba chake ndio sehemu anayoipenda zaidi.

Wakati akituonesha chumba, lilionekana Godoro ambalo mtandao wa Complex umetoa taarifa kuwa lina gharimu kiasi cha (USD 395K) sawa na TSH. Milioni 914. 
Pia walieleza kwamba walizungumza na kampuni ambayo hutengeneza 'vitanda' hivyo na kusema vinadumu sana kuanzia miaka 50 hadi 100.
Kitanda hicho cha magodoro kimetengenezwa na nywele za Punda, Sufu, Pamba na mbegu za Kitani.


EmoticonEmoticon