Habari 5 Kubwa Za Soka Alhamisi April 2

Tetesi za Soka Barani Ulaya Alhamisi April 2

1. Kiungo wa kati wa Manchester United na Ufaransa Paul Pogba amedokeza kuwa kipaumbele chake kwa sasa ni kujiunga na Real Madrid dirisha la usajili litakapofunguliwa, kwasababu nyota huyo wa miaka 27 anataka kuungana na Zinedine Zidane. 

2. Mshambuliaji wa England Marcus Rashford amekiri kuwa anatamani sana kucheza na mshambuliaji mwenzake wa Borussia Dortmund Jadon Sancho, 20, Katina klabu ya Manchester United msimu ujao. 

3. Manchester United wanafuatilia hali ya Thomas Meunier katika klabu ya Paris Saint-Germain huku hatima ya beki huyo wa miaka 28, raia wa Ubelgiji ikiwa haijulikani.

4. West Ham wanajiandaa kuweka dau la kushutukiza la £15m, kumnunua mshambuliaji wa Barcelona na Norway Martin Braithwaite, 28, ambaye amecheza mara tatu pekee tangu alipohamia Nou Camp Januari.

5. Mkufunzi wa Everton Carlo Ancelotti ana matumaini ya kujumuika tena mshambuliaji wa Real Madrid na Colombia James Rodriguez, 28.


EmoticonEmoticon