Habari 5 Kubwa Za Soka Jumanne April 28

Tetesi Za Soka Barani Ulaya Jumanne April 28

1. Manchester United wako tayari kumuuza kiungo wa kati wa Ufaransa Paul Pogba, 27, na kiungo wa kati wa England Jesse Lingard, 27, kumnunua Sancho. 

2. Mkurugenzi wa michezo wa Borussia Dortmund anasema "amenyamaza " kuhusu hatma ya baadae ya Jadon Sancho. Winga huyo wa England, 20, amehusishwa na tetesi za kuhamia Manchester United.

3. Mshambuliaji wa Everton Moise Kean, 20, amehusishwa na tetesi za kuhamia Napoli. Mtaliano huyo huenda akachukuliwa hatua za kinidhamu na Everton kwa kukiuka muongozo wa serikali wa kukabiliana na coronavirus mapema wiki hii. 

4. Wachezaji nyota wa Barcelona Philippe Coutinho, 27, na Ousmane Dembele, 22, wako tayari kujumuishwa kwa mkataba wa kubadilishana wachezaji msimu huu.
Chelsea walimtaka Coutinho lakini sasa wanamnyatia kiungo matata wa Bayer Leverkusen na Ujerumani Kai Havertz, 20.

5. Liverpool wanapigiwa upatu kumsajili mshambuliaji wa Lille Victor Osimhen, 21, ijapo kuwa Leicester na Chelsea pia wanamng'ang'ania raia huyo wa Nigeria .


EmoticonEmoticon