Habari 5 Kubwa Za Soka Jumatano April 08

Tetesi Za Soka Barani Ulaya Jumatano April 08

1. Klabu ya Real Madrid imeahirisha mipango yake ya kumsajili mshambuliaji nyota wa Ufaransa Kylian Mbappe, 21, kutoka Paris Saint-Germain mpaka 2021 kutokana na janga la virusi vya corona.

2. Liverpool imejiunga na msururu wa klabu zinazovutiwa na kutaka kumsajili kiungo wa klabu ya Lille ya Ufaransa Boubakary Soumare, 21. Klabu za Real Madrid, Manchester United, Chelsea na Newcastle pia zinamuwania mchezaji huyo. 

3. Klabu za Arsenal, Chelsea na Celtic wanamuwania mshambuliaji kinda wa Middlesbrough na timu ya taifa ya chini ya miaka 17 ya Jamhuri ya Ireland Calum Kavanagh, 16.

4. AC Milan pia wanaandaa pauni milioni 35 ili kumsajili mshambuliaji wa Arsenal na Uruguay Lucas Torreira, 24.

5. Manchester United bado wanahangaika kutafuta klabu itakayomnunua mshambuliaji wake Alexis Sanchez, 31, kwa kuwa hataki kupunguza mshahara wake. Mshambuliaji huyo wa Chile ambaye yupo kwa mkopo Inter Milan, bado yungali na miaka miwili mpaka mkataba wake na United uishe.


EmoticonEmoticon