Habari 5 Kubwa Za Soka Jumatano April 1

Tetesi za Soka Jumatano April 1
1. Manchester United wanajiandaa kutangaza dau la kumnunua beki wa Juventus na Uholanzi Matthijs de Ligt, 20, huku kiungo wa kati wa Ufaransa Paul Pogba, 27, akiwa tayari kuondoka Old Trafford.
2. Mashetaniwekundu hueda wakalazimika kumlipa mshambuliaji wa Chile Alexis Sanchez, 31, ada ya kila mwaka ya £1.1m atakaporejea kutoka Inter Milan ambako amekuwa akicheza kwa mkopo.
3. Everton wanapanga kuweka dau kubwa la kumnunua mshambuliaji wa Real Madrid na Wales Gareth Bale, 30, msimu wa joto pamoja na kiungo wa kati wa Juventus Aaron Ramsey, 29.
4. Kwa sasa, the Toffees wanatumia huduma ya mawasiliano ya kidigitali ya Zoom inayowakutanisha kwa njia ya video wachezaji na wahudumu wa afya wa klabu hiyo, huku kiungo wa kati wa Ufaransa aliyejeruhiwa Schneiderlin, 30, akijiandaa kuzungumza na mtaalamu wake wa upasuaji kupitia mfumo huo.

5. Mshambuliaji wa Real Madrid Karim Benzema, 32, ametetea kauli yake baada ya kumfananisha mshambuliaji wa Chelsea na mchezaji mwenza wa timu ya taifa ya Ufaransa Olivier Giroud, 33, 'gari dogo linaloenda kasi lakini halina nguvu'alipofanya Instagram live. 


EmoticonEmoticon