Habari 5 Kubwa Za Soka Jumatatu April 27

Tetesi Za Soka Barani Ulaya Jumatatu April 27
1. Kiungo wa kati wa Barcelona Philippe Coutinho, ambaye yuko kwa mkopo Bayern Munich, aliambiwa na Liverpool kuwa hawana mpango wa kumsajili tena mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil wa miaka 27- walipokuwa wanajadili uwezekano wake kurejea katika klabu hiyo.
2. Arsenal wamejiondoa katika mazungumzo ya mkataba wa mshambuliaji Pierre-Emerick Aubameyang. Kiungo huyo wa kimataifa wa Gabon mwenye umri wa miaka 30-anatarajiwa kuondoka katika uwanja wa Emirates, huku klabu za Manchester United, Inter Milan, Barcelona, Real Madrid na Chelsea zikitaka kumsaini.
3. Kipa wa Manchester United, Mhispania David de Gea,29, amesema kuwa anataka kusalia Old Trafford kwa "miaka mingi" lakini nafasi yake inakabiliwa na ushindani kutoka kwa Muingereza Dean Henderson, 23, ambaye ameonesha umahiri wake baada ya kusajili kwa mkopo kutoka Sheffield United.

4. Ajenti wa zamani wa Neymar, Wagner Ribiero amesema mshambuliaji huyo wa Brazil na Paris St-Germain, 28, alitaka kujiunga na Chelsea alipokuwa na miaka 17.

5. Mkufunzi wa Chelsea Frank Lampard amezungumza na mshambuliaji wa Napoli Dries Mertens na anatarajia kumpata kiungo huyo wa Ubelgiji wa miaka 32, kwa uhamisho wa bure. 


EmoticonEmoticon