Habari 5 Kubwa Za Soka Jumatatu April 6

Tetesi Za Soka Barani Ulaya Jumatatu April 6


1. Kiungo wa kati wa Manchester City na Uhispania David Silva, 34, huenda akapatiwa mechi ya mwisho ya kumuaga katika uwanja wa Etihad mwisho wa msimu iwapo mlipuko wa coronavirus utamzuia kuwaaga mashabiki wa klabu hiyo baada ya kuichezea klabu hiyo kwa miaka 10 kitu ambacho kimemsaidia kushinda taji la ligi kuu mara. 

2. Leicester, Newcastle, Crystal Palace na Aston Villa wana hamu ya kumsajili mshambuliaji wa Rangers na Colombia Alfredo Morelos, 23.

3. Real Madrid inataka kumsaini mshambuliaji wa Tottenham na England Harry Kane mwenye umri wa miaka 26.

4. Mshambuliaji wa Borussia Dortmund na timu ya taifa ya England Jadon Sancho, 20, amekataa uhamisho wa kuelekea Manchester United mwisho wa msimu huu iwapo watashindwa kufuzu katika michuano ya klabu bingwa.

5. Klabu za ligi ya Premia zimenunua vifaa vyao vya kupima virusi vya corona huku kukiwa na hofu kwamba mechi zitachezwa bila mashabiki.


EmoticonEmoticon