Hatimaye Ronaldinho Na Kaka Yake Watoka Gerezani Baada Ya Msoto Wa Siku 32

Staa wa zamani wa FC Barcelona na timu ya taifa ya Brazil Ronaldinho na kaka yake Assis wamepata dhamana na kutoka gerezani nchini Paraguay baada ya kukaa huko kwa siku 32.
Ronaldinho na Kaka yake wamepata dhamana kwa dola milioni 1.6 (Tsh Bilioni 3.7) baada ya awali kukataliwa dhamana nyepesi kwa hofu wangeweza kutoroka.
Pamoja na kupata dhamana hiyo lakini jaji Gustavo Amarilla ameamuru wawili hao kutolewa gerezani na kwenda kuishi katika nyumba/hotel katika mji wa Asuncion wakiwa chini ya uangalizi maalum.
Ronaldinho na Assis walikamatwa na Polisi nchini Paraguay kwa tuhuma za kuingia nchini humo na Passport za Paraguay ambazo zinawaonesha wao kama raia wa nchi hiyo wakati ni raia wa Brazil.
Utetezi wa Ronaldinho wa awali unadaiwa kueleza kuwa staa huyo na kaka yake waliingia Paraguay kwenda kufanya tangazo na hati hizo bandia za kusafiria walipewa kama zawadi na rafiki yao waliyekuwa wanakwenda kufanya nae kazi.


EmoticonEmoticon