Jarida La Forbes Lamtaja Kanye West Kama Bilionea, Kanye Awachana Hawajui Kuhesabu

Hatimaye Kanye West ametajwa na jarida la Forbes kama Bilionea, hii ni baada ya kuvutana mwaka mzima.

Kama utakumbuka, mwaka jana jarida la Forbes lilishindwa kumtaja Kanye West kama Bilionea licha ya kuwaonesha Risiti kuwa ana utajiri wa ($890m)

Kwa mujibu wa taarifa mpya iliyotoka jana Ijumaa, Forbes wamempa Kanye hadhi ya Bilionea wakidai ana utajiri wa ($1.3 billion) ambazo ni sawa na Trilioni 3 za Kitanzania. Hii imetokana na kampuni yake ya Yeezy inayohusika na mavazi pamoja na viatu.

Timu ya Kanye iliwasilisha nyaraka muhimu za kifedha kwenye uongozi wa Jarida hilo kuthibitibisha utajiri wake na hata hivyo Kanye hajawaacha Forbes, amewachana kwamba hawajui kuhesabu kwani yeye ana utajiri wa ($3.3 Billion)


EmoticonEmoticon