Kwa Mara Ya Kwanza Burundi Yatangaza Visa Zaidi Ya Kimoja Cha Corona

Waziri wa afya nchini humo Thadée Ndikumana, ametangaza watu wawili ambao ni raia wa Burundi kuwa na maambukizi ya virusi vya corona.
Raia hao ambao wote ni wanaume, mmoja ana umri wa miaka 56 huku mwingine ana umri wa miaka 42, na walikuwa wanawasili kutoka Rwanda na Dubai, Waziri alisema.
Naye msemaji wa rais wa Burundi, bwana Jean Claude Karerwa aliongea na BBC siku kadhaa zilizopita na kusema kuwa Mungu atawalinda na maambukizi haya kwa sabbu Mungu ameiweka serikali ya Burundi ka tika sehemu ya kipekee.
Taifa la Burundi linatarariwa kuwa na uchaguzi mkuu wa rais tarehe 20 Mei.
Bwana Karerwa alisema kuwa uchaguzi unaweza kuwa na mabadiliko kama tu maambukizi hayo ya Covid 19 yatazidi nchini humo.
Licha ya kwamba Burundi ilikuwa haijathibitisha kuwa na maambukizi , lakini ilikuwa hatua za kudhibiti ugonjwa huo kwa kusitisha ndege zote kwa muda wa siku saba.


EmoticonEmoticon