Mapendekezo Ya Premier League Kuhusiana Na Kupunguza Mishahara Ya Wachezaji Baada Ya Kikao Siku Ya Ijumaa

Baada ya kufanya kikao na uongozi wa vilabu ijumaa,usimamizi wa Premier league ulipendekeza kuwa wachezaji wa vilabu vyote vinavyoshiriki katika ligi hiyo kukubali kupunguza mishahara yao kwa sasilimia 30,ikiwa ni njia mojawapo tu ya kuchanga pesa za kusaidia serikali kukabiliana na janga la Corona.

Taarifa kutoka kwa Premier league imesema kuwa ilikuwa inafahamu changamoto ambazo vilabu zinapitia wakati huu ambao ligi hiyo imesitishwa,kwa hivyo kama njia ya kusadia wachezaji wengi kutopoteza ajira msimu huu ambao biashara nyingi zimefungwa ni vyema wapunguze mishahara yao.

Tangazo hili linajiri wakati wachezaji wengi kama vile Neymar,Christiano Ronald na Messi wakiendelea kutoa michano katika mataifa yao ili kusaidia serikali zao kukubaliana na virusi hivyo.


EmoticonEmoticon