Mfalme Ajifungia Karantini Na Wanawake 20 Kisa Corona

Mfalme wa Thailand Maha Vajiralongkorn,  aka  Rama X ameripotiwa kujifungia kwenye karantini na wanawake 20  umbali wa kilomita zaidi ya elfu nane kutoka nyumbani.

Taifa hilo limesajili visa 1,651 huku visa 17 vikisajiliwa Jumanne pekee  na watu 10 wakiaga dunia kwa ajili ya coronavirus. 

Kiongozi huyo mzushi  amekuwa akijitenga katika hoteli moja ya kifahari  katika mji wa  Garmisch-Partenkirchen  na ujumbe wake, jarida la The Independent  limeripoti.

Mfalme huyo pamoja na msafara wake wamechukua  hoteli nzima  ya Grand Hotel Sonnenbichl  baada ya hoteli hiyo kupata idhini ya kuruhusu msafara wake. 

Miongoni mwa walioandamana naye ni  wanawake 20 wa kumpa raha zake  na wafanyikazi kadhaa.

Gazeti la ujerumani  Bild, limesema hadi sasa haijafahamika  iwapo wake zake wanne pia wapo katika hoteli hiyo.


EmoticonEmoticon