New Zealand Imeweza Kuzuia Maambukizi Ya Corona


New Zealand inasema kwamba imezuia maambukizi ya Covid 19 katika jamii hatua ambayo inamaanisha kwamba wameangamiza virusi hivyo.
Huku wagonjwa wapya wachache wakiripotiwa katika siku kadhaa - mmoja siku ya Jumapili - Waziri mkuu Jacinda Ardem amesema kwamba virusi hivyo vimeangamizwa kabisa.
Lakini maafisa wameonya dhidi ya kupunguza kasi dhidi ya virusi hivyo, wakisema kwamba haimaanishi kwamba visa vya ugonjwa huo vimeisha kabisa.
Habari hiyo inajiri saa chache kabla ya New Zealand kuondoa masharti yake makali ya kukaribiana miongoni mwa raia wake.
Kuanzia Jumanne , biashara zisizo na muhimu mkubwa , huduma za Afya na elimu zinatarajiwa kufungua milango yake tena.
Watu wengi hatahivyo watatakiwa kusalia majumbani kila wakati na kuzuia kukaribiana.
"Tunaufungua uchumi , lakini haturuhusu mikusanyiko ya watu'' , bi Arden alisema katika hotuba hiyo ya serikali ya kila siku kwa umma. News Zealand imeripoti chini ya wagonjwa 1,500 na vifo 19 .
Mkurugenzi mkuu wa Afya nchini New Zealand Ashley Bloomfield alisema kwamba wagonjwa wachache wanaoripotiwa katika siku za hivi karibuni wanatupatia motisha kwamba tunaafikia lengo letu la kuangamiza ugonjwa huu.


EmoticonEmoticon