Taifa La Ethiopia latangaza Hatua Ya Kusitisha Shughuli Zote Nchini Humo Kufuatia Ongezeko La Corona

Taifa la Ethiopia, Afrika Mashariki, limekuwa la hivi punde kutangaza hatua ya serikali ya kusitisha shughuli zote nchini humo kama njia ya kupunguza kuenea kwa virusi vya Corona.

Kwa sasa Ethiopia [Uhabeshi] limesajili visa 52 vya maambukizi kufikia siku ya Jumatano huku watu 2 wakiripotiwa kufariki kutokana na virusi hivyo na watu wengine 4 wakiwa wamepata nafuu na kuruhusiwa kuondoka hospitalini.

Taifa la Kenya Ukanda wa Afrika Mashariki lingali linaongoza kwa asilimia kubwa ya maambukizi huku watu 179 wakiwa wameambukizwa virusi vya corona, 6 wameaga dunia huku tisa wakipona na kuruhusiwa kurejea nyumbani.
Credit:radiojambo


EmoticonEmoticon