Zari Awapiga Vijembe Maslay Queen, Kipindi Hiki Cha Corona Hakuna Madanga Na Hoteli Zimefungwa

Bata analokula mwanamama Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ na wanawe wakati akituikia kipindi cha kukutoka ndani (lockdown) huku Afrika Kusini ni balaa.

Pamoja na kulalamika kuwa kipindi hiki kimemfanya kuwa kama mfungwa, lakini amekuwa akiachia picha video kwenye mitandao ya kijamii vikimuonesha akijiachia kwa raha zake na wanaye.

Zari ni mama wa watoto watano ambao ni Pinto, Raphael na Quincy aliozaa na aliyekuwa mumewe, marehemu Ivan Ssemwanga na Tiffah na Nillan aliozaa na staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Mondi’.

Serikali ya Afrika Kusini iliingia lockdown ya siku 21 ili kudhibiti maambukizi ya Corona yaliyokuwa yanaongezeka kwa kasi.

Baada ya hapo jeshi lilianza kazi yake ya kuzuia watu kusambaa mitaani na kutii agizo la Serikali ya Afrika Kusini.
Kwa upande wake Zari aliingia lockdown na wanaye na kuendeleza bata zake za kufa mtu kwani mjengo anaoishi huko Durban, Afrika Kusini una kila kitu ndani yake.

Amekuwa akiachia video na picha akiwa kwenye kitanda baab’kubwa na wanawe wakiangalia bonge la runinga kisha wakiogelea kwenye bwawa lililopo ndani ya nyumba hiyo huku wakila na kunywa.

Wakati akifanya hao, Zari ametumia kurasa zake za mitandao ya kijamii kuwananga warembo wanaodanga akiwaambia safari hii watakiona cha moto kutokana na janga la Corona.

Zari amekuwa akiwatupia madongo warembo waliokuwa wakirundikana kwenye mahoteli ya kifahari kuwinda wanaume kwamba, sasa watawinda nini kwani hata mahoteli hayo yamefungwa.

Zari anasema warembo hao maarufu kwa jina la slay queen wamekuwa wakimponda kuwa anaishi maisha feki, lakini sasa wanatakiwa wajitazame kati yao na yeye ni nani anaishi maisha feki.

“Kwani hamruhusiwi kupiga picha kwenu? Wakitoka utawasikia wakisema Zari anafeki maisha.
“Angalieni maisha yenu sasa. Mungu awanusuru. Mimi tayari nimebarikiwa,” aliandika Zari.

Zari anatumia kipindi hiki cha lockdown kuonesha ufahari uliopo kwenye kila kona ya mjengo wake huo kama sehemu ya kuwadorishia mahasimu wake kwenye mitandao ya kijamii.


EmoticonEmoticon