Bow Wow Kuachana Na Muziki Baada Ya Album Yake Ya Mwisho, Atangaza Hatua Nyingine Inayofwata

Baada ya kuihudumia game ya muziki kwa takribani miaka 20, Bow Wow ametangaza hatua nyingine kwenye muziki wake.

Bow Wow ambaye aliachia ngoma yake ya kwanza "Bounce With Me" mwaka 2000 amesema anafikiria kuacha muziki na kujikita kwenye familia na malezi ya mtoto wake Shai Moss muda wote.
"Ndio, Ninataka kumfanya mwanangu Shai kuwa tayari, anataka kufuata nyayo zangu hivyo inanilazimu kubadili harakati zangu. Anaoneka kuja kuwa nyota mkubwa! 

Tunakwenda kumiliki televisheni na filamu. Muunganiko wa mtoto na baba, kama hakuna mwingine." aliandika Bow Wow kwenye twitter akimjibu shabiki mmoja ambaye aliuliza kama anafikiria kuacha muziki baada ya kuachia album yake ijayo.

Album yake ijayo itakuwa ya pamoja na Omarion ambayo ameitaja kwamba itaachiwa hivi karibuni japo hana uhakika sana.

Tangu akutane na Jermaine Dupri mwaka 1998 na kumnyoosha kimuziki hadi kuachia album yake ya kwanza 'Beware of Dog' Bow Wow tayari ameachia jumla ya albums 6, singles 26 na mixtape 7.


EmoticonEmoticon