Burundi Wamtangaza Mshindi Wa Uraisi Baada Ya Uchaguzi

Tume ya Uchaguzi nchini Burundi imemtangaza mgombea wa chama tawala nchini humo cha CNDD –FDD Evariste Ndayishimiye kuwa mshindi wa kiti cha urais kufuatia uchaguzi uliofanyika wiki iliyopita.
Ndayishimiye ambaye ni Jenerali Mstaafu ameshinda kwa kupata asilimia 68.72 ya kura zote zilizopigwa, wakati Agathon Rwasa kutoka chama kikuu cha upinzani akipata asilimia 24.19 ya kura hizo.
Kwa kuwa Jenerali Ndayishimiye amepata zaidi ya asilimia hamsini ya kura, uchaguzi huo umeepuka kufanyika kwa duru ya pili.


EmoticonEmoticon