Burundi Wanafanya Uchaguzi Wa Kumchagua Rais Leo Mei 20

Hatimaye Uchaguzi Mkuu wa Burundi uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu huku ukielezwa kuwa ni mwanzo mpya wa Demokrasia katika nchi hiyo, unafanyika leo Mei 20, 2020 baada ya miaka 15 ya Uongozi wa Rais Pierre Nkurunziza.

Wachambuzi wa masuala ya siasa, kijamii na kidiplomasia, wameshauri Serikali mpya itakayochaguliwa kuandaa mjadala wa Kitaifa ili kubaini matatizo na changamoto za wananchi na kuzifanyia kazi.

Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), imesema haitapeleka waangalizi wake kutokana na masharti yaliyotolewa na Serikali ya nchi hiyo kuwa waangalizi watatakiwa kukaa karantini siku 14 ambazo zitamalizika wakati uchaguzi huo umeshafanyika.

Kuna wagombea 7 wa nafasi ya urais, lakini ni wawili tu wanaobashiriwa kuwa na uwezekano wa kuchaguliwa. 

Ambao ni Evariste Ndayishimiye, Katibu Mkuu wa Chama cha CNDD-FDD na Agathon Rwasa, Kiongozi wa Chama Kikuu cha Upinzani cha CNL.


EmoticonEmoticon