CORONA : Hospitali Za Uingereza Zaanza Kufanyia Majaribio Dawa Mpya

Kaye Flitney ni mmoja wa watu waliojitolea kujumuishwa katika majaribio ya dawa mpya ya kukabiliana na virusi vya corona.
Dawa mpya iliotengenezwa na wanasayansi wa Uingereza kutibu Covid 19 inafanyiwa majaribio katika chuo kikuu cha Southampton.
Ikiwa imetenegenezwa na kampuni ya Synairgen , inatumia protini kwa jina infterferon beta, ambayo hutoka katika mwili wa binadamu anapopata maambukizi ya virusi.
Matokeo ya majaribio hayo yanatarajiwa kutolewa mwishoni mwa mwezi Juni.
Kwa sasa kuna dawa chache zinazoweza kutibu virusi hivyo huku madaktari wakitegemea kinga ya wagonjwa wao.
Je ni dawa gani hiyo?
Interferon beta ni dawa inayolinda mwili wa binadamu dhidi ya virusi, ikionya dhidi ya shambulio la virusi , kulingana na Richard Marsden , afisa mkuu mtandaji wa kampuni ya Synairgen iliopo na makao yake mjini Southampton.
Anasema kwamba virusi vya corona hujaribu kukabiliana na uzalishaji wake kama mpango wa kutaka kukwepa mfumo wa kinga mwilini.
Dawa hiyo ina muundo maalum wa interferon beta inayowekwa moja kwa moja kwenye njia za hewa wakati zilizopo na virusi, kwa matumaini kwamba kipimo cha protini moja kwa moja kitatoa majibu ya kupambana na virusi hata miongoni mwa wagonjwa ambao kinga zao tayari ni dhaifu.
Interferon beta hutumika sana kutibu ugonjwa wa kupooza. Synairgen tayari imethibitisha kwamba maandalizi yake yanaweza kuimarisha kinga katika mapafu ya mgonjwa mwenye asthma na magonjwa sugu ya mapafu.
Lakini tunaweza kujua iwapo inaweza kukabiliana na Covid-19 baada ya kufanyiwa majaribio kadhaa miongoni mwa binadamu.
Credit:Bbc


EmoticonEmoticon