CORONA : Hoteli Nchini Nigeria Zavunjwa

Maafisa nchini katika jimbo lenye utajiri wa mafuta la Rivers nchini Nigeria wamevunja hoteli mbili kufuatia madai ya kukiuka sheria za kukaa nyumbani zilizowekwa kwa lengo la kudhibiti kusambaa kwa virusi vya corona.
Gavana wa jimbo hilo Nyesom Wike, ambaye alisimulia kuvunjwa kwa Hoteli ya Edemete Hotel na Prodest Home Jumapili, alisema kuwa waliofanya shughuli hiyo walikuka maagizo kwamba hoteli zinapaswa kufungwa.
Alisema kuwa watu waliopatikana na virusi vya corona walipatikana katika hoteli mbali mbali katika jimbo hilo. Lakini hakusema iwapo yeyote ambaye ana maambukizi ya Covid-19 amekuwa akiishi katika hoteli hizo mbili zilizovunjwa.
'Tulikataa kutoa hongo'
Mameneja wa hoteli zote mbili wamekamatwa, lakini mmiliki wa Prodest Home amekana kwamba hoteli yake ilikua imefunguliwa.
"Hoteli haikua ikifanya kazi na 70% ya wahudumu walikua wamerudishwa nyumbani ," Gogorobari Promise Needam alioiambia BBC.
"Kulikua na watu watatu tu katika hoteli.
"[Maafisa ] walikuja na walikua wakiomba rushwa wakasema watatuacha tuendelee kufanya kazi, kama tutawapatia pesa lakini tukawambia hatufanyi kazi kwa hiyo hatuna pesa za kuwapatia ," alisema .
Serikali ya jimbo la Rivers amekanusha shutuma hizo.


EmoticonEmoticon