CORONA : Kenya Yafikisha Jumla Ya Wagonjwa 758

Kenya yasajili visa vingine 21 vipya vya maambukizi ya Corona na idadi ya wote walioathiriwa na ugonjwa huo kufikia watu 758. 
Katibu katika wizara ya afya Mercy Mwangangi athibitisha.

Wagonjwa 2 wa virusi vya Corona waaga dunia na idadi ya walioaga kufuatia ugonjwa huo kufikia watu 42. Waathiriwa wengine 3 wa Corona wapata nafuu na idadi ya wote waliopona kupanda hadi watu 284 humo nchini.


EmoticonEmoticon