CORONA : Kenya Yasajili Visa Vipya 25 Jumla 912

Serikali ya Kenya imetangaza ongezeko la wagonjwa wa Corona nchini humo ambapo sasa inafikia 912 baada ya ongezeko la wengine 25 leo Mei 18, 2020.

Katibu Mkuu wa Tawala za Afya Rashid Aman ametangaza ongezeko hilo huku akisema kuwa Kati ya wagonjwa hao, 23 ni wanaume wakati wawili ni wanawake na umri wao ni kati ya miaka 22 hadi 50.

Katika kesi hizo 25 mpya kesi 23 ni Raia wa Kenya na wawili ni Wasomali huku Dk Aman akweka wazi kuwa mpaka sasa sampuli 44,851 zimepimwa nchini humo.


EmoticonEmoticon