CORONA : Shirika La Afya Duniani (WHO) Laonya Kuhusiana Na Matumizi Ya Dawa Za Miti Shamba

Shirika la Afya Duniani limesihi watu kutoweka imani zao kwa dawa za mitishamba zinazotengenezwa na wenyeji kwa misingi ya kudai kukabiliana na virusi vya corona.

Hatua hiyo inawadia wakati ambapo marais karibu wanne wa Afrika wamesema wanaagiza kiasi kikubwa cha dawa ya mitishamba iliyosemekana kupatikana huko Madagascar kuwa ina uwezo wa kutibu virusi vya corona.

Dawa za mitishamba ambazo mara nyingi hupatikana katika eneo huchangia pakubwa katika suala la afya kote barani Afrika.

Shirika la Afya Duniani limepata taarifa na kutoa onyo hilo wakati ambapo kila mmoja duniani ana hamu ya kupata dawa ya kutibu virusi vya corona.

Shirika la Afya Duniani limesema ni muhimu dawa zinazosemekana kuwa na uwezo wa kutibu kufanyiwa majaribio kwanza na kuonya kuwa huenda watu wakaona wamepata tiba na kujihisi kuwa salama ikiwa watakuwa na imani na dawa ambazo hazijafanyiwa majaribio.

Dawa hiyo inayohusishwa na mmea wa Kichina unaoitwa Artemisia(pakanga)-ambao ni mojawapo ya miti ambayo huchanganywa pamoja na mimea mingine ya Madagascar kama tiba ya ugonjwa wa Malaria.

Hayo yanajri wakati Rais wa Madagascar akisema nchi yake itaanza majaribio ya kitabibu ya kinywaji cha mitishamba ambacho anakipigia upatu kuwa kinauwezo wa kuzuia na kutibu corona.

Rais Andry Rajoelina amesema majaribio hayo yataanza wiki ijayo.

Pia amewataka wananchi wa taifa hilo kupanda kwa wingi mmea ambao unatomika kutengeneza kinywaji hicho. Kilichopewa jina la Covid-Organics.

Rais Rajoelina amesema kwa sasa anatafuta kibali cha WHO ili wathibitishe kinywaji hicho kuwa dawa.

Hata hivyo msimamo wa WHO kuhusu kinywaji hicho mpaka sasa haujabadilika na wanaonya watu dhidi ya dawa mbadala kutumika kama kinga ama tiba ya corona.

Mpaka kufikia sasa, watu zaidi ya milioni 3.5 duniani kote wamethibitishwa kupata maambukizi ya virusi vya corona, watu zaidi ya 250,000 (laki mbili na hamsini) wamefariki dunia huku watu zaidi ya milioni moja wakipona.
Chanzo:Bbc


EmoticonEmoticon