CORONA : Uingereza Imeruhusu Matumizi Ya dawa Ya Kukabiliana Na Virusi Ya Remdesivir

Tiba ambayo inaonekana kupunguza muda wa kupona unapopata virusi vya corona imeanza kupatikana katika hospitali za Uingereza.
Dawa ya Remdesivir ina kabiliana na virusi ambayo awali ilikuwa imetengenezwa kutibu viusi vya Ebola.
Wadhibiti nchini Uingereza wanasema kwamba kuna ushahidi wa kutosha wa kuidhinisha matumizi ya dawa hiyo kwa wagonjwa walio hospitali.
Kwa sababu ya muda na hali ilivyo, itawaendea wale wenye uhitaji zaidi.
Marekani na Japani pia nazo tayari zimeshafanya maandalizi ya kupata dawa hiyo mapema kabla ya kufikiwa kwa makubaliano ya kibiashara juu ya dawa hiyo.
Kwa sasa dawa hiyo inafanyiwa majaribio kote duniani ikiwemo Uingereza.
Takwimu za awali zinaonesha kwamba dawa hiyo ina uwezo wa kupunguza siku za kupona hadi nne.
Bado haijafahamika kampuni ya dawa ya Gilead Sciences ina dawa hizo kiasi gani kwa ajili ya wagonjwa wa Uingereza.
Namna ya matumizi yake itategemea kulingana na ushauri wa daktari.


EmoticonEmoticon