Habari 5 Kubwa Za Soka Alhamisi May 7

Tetesi Za Soka Barani Ulaya Alhamisi May 7
1. Manchester United wanataka kuongeza mkataba wa mkopo wa mshambuliaji wa Nigeria Odion Ighalo, 30 , kutoka Shanghai Shenhua.
2. Liverpool, Southampton na RB Leipzig wanamuwania winga wa Werder Bremen Milot Rashica, 23, ambaye mkataba wake utakwisha mwezi Juni.
3. Matumaini yaArsenal ya kumsajili beki wa kushoto Layvin Kurzawa kutoka Paris St-Germain yamezimika , mchezaji huyo atamwaga wino kukipiga katika klabu ya Barcelona. 
4. Liverpool na Manchester City wanavutiwa na kiungo wa kati Mbelgiji Aster Vranckx,17, anayechezea KV Mechelen.
5. Washika bunduki wanapendelea kumsajili mchezaji wa RB Leipzig, Dayot Upamecano, 21, kiwapiku Tottenham na Manchester United, ambao pia wanamtomlea macho mchezaji huyo anayecheza nafasi ya ulinzi .


EmoticonEmoticon