Habari 5 Kubwa Za Soka Alhamisi Mei 21

Tetesi Za Soka Barani Ulaya Alhamisi Mei 21

1. Liverpool wako tayari kuwauza wachezaji watatu msimu huu ili kuweza kugharamia uhamisho wa pauni milioni 52 kwa ajili ya mshambuliaji wa miaka 24 wa RB Leipzig, mjerumani Timo Werner.

2. Mshambuliaji wa Manchaster City, mjerumani Leroy Sane, 24, ametengewa jezi nambari 10 katika kikosi cha Bayern Munich kwa ajili ya msimu ujao.

3. Manchester United wangependa kumshikilia mshambuliaji, 30, Odion Ighalo,kwa mkopo kutoka Shanghai Shenhua, lakini ''wamerudi nyuma'' kuhusu mustakabali wa mchezaji huyo raia wa Nigeria baada ya Marcus Rashford afya yake kuimarika.

4. Chelsea wanapambana kumuuza Victor Moses wakati Inter Milan wakikataa kulipa kitita cha pauni milioni 10.75, kwa jailli ya winga huyo wa Nigeria , 29.

5. Neymar, 28, hataondoka Paris St-Germain kujiunga tena na Barcelona msimu huu kwasababu ya athari za virusi vya corona kwa uchumi wa vilabu vya mpira, ameeleza wakala wa mbrazili huyo.


EmoticonEmoticon