Habari 5 Kubwa Za Soka Alhamisi Mei 28

Tetesi Za Soka Ulaya Alhamisi Mei 28

1. Liverpool wanataka kumsaini winga wa Wolves na Uhispania Adama Traore, 24, huku mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp akiripotiwa kuwasiliana na mchezaji huyo moja kwa moja.

2. Manchester United na Real Madrid wanataka kumsaini kiungo wa kati wa Rennes Ufaransa Eduardo Camavinga, 17.

3. Liverpool haitalipa ada ya £50m itakayomwezesha mshambuliaji wa RB Leipzig na Ujerumani Timo Werner, 24, kujiunga nao wakikadiria kuwa thamani yake ni £30m katika soko la sasa la uhamisho.

4. Mshambuliaji wa Nigeria Odion Ighalo, 30, ametoa ombi la kibinafsi kwa klabu ya china ya Shanghai Shenhua, la kutaka kurefusha mkataba wake wa mkopo Manchester United. 

5. Mkufunzi wa Tottenham Jose Mourinho klabu hiyo "haitatumia fedha nyingi" awamu ijayo ya uhamisho wa wachezaji.


EmoticonEmoticon