Habari 5 Kubwa Za Soka Ijumaa May 8

Tetesi Za Soka Barani Ulaya Ijumaa May 8

1. Klabu ya Newcastle itatumia pauni milioni 70 kumsajili mchezaji wa nafasi ya kiungo wa Barcelona, raia wa Brazil Philippe Coutinho ikiwa pendekezo la klabu hiyo kununuliwa litafanikiwa. 
Mchezaji huyo mwenye miaka 27 anaichezea Bayern Munich kwa mkopo.

2. Arsenal wanaweza kupewa nafasi ya kumsajili mshambuliaji wa Inter Milan Mauro Icardi, 27, ikiwa ni mbadala wa mshambuliaji Pierre- Emerick Aubameyang, 30.

Mkataba wa Aubameyang unatarajiwa kumalizika msimu ujao, wakati Icardi anacheza kwa mkopo Paris St-Germain.

3. Borussia Dortmund wanategemea winga wa England Jadon Sancho, 20, kuendelea kubaki kwenye klabu hiyo, ingawa Manchester United pia imeonesha nia ya kumtaka mchezaji huyo.

4. Kampuni ambayo inaelekea kuwa wamiliki wapya wa Newcastle pia inataka kumsajili beki wa kati wa Napoli na Senegal Kalidou Koulibaly, 28. Mchezaji huyo anatarajiwa kuondoka kwenye klabu hiyo ya Italia kwa kitita cha pauni milioni 69.8. 
Hata hivyo, Koulibaly anafikiria kuhamia Liverpool. 

5. Mchezaji wa miaka 16, wa klabu ya Barcelona Marc Jurado ametupilia mbali ofa kuchezea klabu hiyo ya Uhispania. Beki huyo wa kulia anajiandaa kujiunga na Manchester United.


EmoticonEmoticon