Habari 5 Kubwa Za Soka Ijumaa Mei 22

Tetesi Za Soka Barani Ulaya Ijumaa Mei 22

1. Barcelona wamepunguza bei ya kumuuza beki wao wa kati Samuel Umtiti, 26, mpaka kufikia pauni milioni 27 tu, wakati huu ambapo klabu za Manchester United na Arsenal zinamnyatia mchezaji huyo.

2. Man United wameazimia kuwa kusajili beki mpya wa kati kuwa ni suala la kipaumbele kwa dirisha lijalo la usajili huku kocha Ole Gunnar Solskjaer akiamini sasa ana nafasi nzuri Zaidi ya kumnasa beki wa Napoli na Senegali Kalidou Koulibaly, kwa kuwa PSG imeacha kumfuatilia. 

3. Real Madrid na Manchester United huenda wakatakiwa kusubiri mpaka miaka miwili ijayo ili kumsajili mshambuliaji wa Borussia Dortmund Erling Haaland, 19, kwa kuwa mkataba wake wenye kifungu cha bei cha dola milioni 75 unasema anaweza kuuzwa kuanzia 2022 na si chini ya hapo.

4. Kiungo wa Juventus na Bosnia-Herzegovina Miralem Pjanic, 30, anatarajiwa kukataa kuhamia Ligi ya Primia mwishoni mwa msimu, huku Cchelsea ikitajwa kama moja ya klabu ambazo ilikuwa ikimtolea macho.

5. Paris St-Germain bado wana nia ya kumsajili mshambuliaji wa Arsenal na Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, 30, ambaye amesalia na mwaka mmoja tu katika mkataba wake wa sasa na Arsenal. 


EmoticonEmoticon