Habari 5 Kubwa Za Soka Ijumaa Mei 29

Tetesi Za Soka Ulaya Ijumaa Mei 29
Tetesi Za Soka Ulaya Ijumaa Mei 29
1. Leicester wamempatia kiungo wa kati wa Liverpool Adam Lallana, ofa ya mkataba wa kudumu. Mkataba wa kiungo huyo wa kimataifa wa England, Anfield unakamilika mwisho wa mwezi Juni.
2. Klabu tano za ligi ya Premia - Chelsea, Newcastle, Manchester United, Arsenal na Leicester - zinamtaka kiungo wa kati wa Barcelona na Brazil midfielder Philippe Coutinho. Nyota huyo wa miaka 27, ambaye kwa sasa yuko Bayern Munich kwa mkopo, anatarajiwa kuuzwa kwa karibu £90m. 
3. Real Madrid wamepokea ofa kutoka kwa klabu zinazomtaka mshambuliaji wa Wales Gareth Bale,30, lakini mchezaji huyo anatarajiwa kusalia katika klabu hiyo kwa mwaka mwingine mmoja.
4. Manchester United na Newcastle wanamtaka winga wa Uruguay Facundo Pellistri,18, ambaye kwa sasa anachezea klabu ya Penarol.
5. Mshambuliaji wa England Jadon Sancho ametatizika na tetesi kwamba anataka kuhama Borussia Dortmund, amesema mchezaji mwenzake Thomas Delaney. Sancho, 19, anahusishwa na uhamisho wa kuenda Manchester United.


EmoticonEmoticon