Habari 5 Kubwa Za Soka Jumanne May 5

Tetesi Za Soka Barani Ulaya Jumanne May 5

1. Mshambuliaji wa Brazil Neymar, 28, yungali anataka kuihama PSG na kurejea Barcelona na inaaminika kuwa yupo tayari kukatwa mshahara kwa silimia 50 ili kutimiza azma yake ya kurudi Uhispania.

2. Real Madrid wanajipanga kutuma ofa ya kumsajili mkiungo wa Man United na Ufaransa, Paul Pogba, 27.

3. Liverpool wamewaambia wawakilishi wa Timo Warner,24, kuwa wanahitaji muda zaidi ili kuamua kama watatuma ofa kwa mshambuliaji huyo wa RB Leipzig, katika kipindi hiki ambacho wanasubiri kutathmini athari za ugonjwa wa corona katika dirisha la usajili.

4. Kiungo wa Sao Paulo ya Brazil Igor Gomez ,21, pia anawindwa na Real Madrid, lakini klabu yake haijapokea ofa rasmi. Vilabu vya Barcelona, Sevilla na Ajax pia vinaripotiwa kummezea mate. 

5. Newcastle itawalazimu kuilipa Tottenham pauni milioni 12.5 kama watataka kumsajili kocha Mauricio Pochettino mwezi huu, lakini hawatatoa hata senti moja wakimchukua baada ya Mei 31.


EmoticonEmoticon