Habari 5 Kubwa Za Soka Jumanne Mei 19

Tetesi Za Soka Barani Ulaya Jumanne Mei 19

1. Juventus wanaweza kuuza wachezaji kadhaa akiwemo kiungo wa Bosnia Miralem Pjanic, 30 na mshambuliaji wa Argentina Gonzalo Higuain, 32, msimu huu kama sehemu ya sera mpya ya kifedha ili kuisaidia klabu kukabiliana na atahri za kiuchumi zilizosababishwa na janga la corona.
2. Kiungo wa Bayer Leverkusen Kai Havertz anapaswa kukataa nafasi ya kwenda Liverpool na badala yake ajiunge na Borussia Dortmund, anashauri mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Ujerumani Jens Nowotny.
3. Barcelona wanatarajia kuongeza juhudi katika kuhakikisha wanamsajili mshambuliaji wa Inter Milan na Argentina Lautaro Martinez, 22.
4. Manchester United wako tayari kurejesha tena nia yao ya kumsajili mchezaji wa nafasi ya ulinzi wa klabu ya Napoli, msenegali Kalidou Koulibaly, 28 baada ya kubaini kuwa Liverpool inamtupia macho nyota huyo.
5. Mlinda mlango wa Liverpool Loris Karius, 26, hatarejea kufanya mazoezi na klabu hiyo kwa muda.Raia huyo wa Ujerumani amesitisha mkataba wake na klabu yake ya mkopo Besiktas mapema mwezi huu.


EmoticonEmoticon